Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Peter Kairo ametoa wito kwa wakenya msimu huu wa pasaka kuiga mfano wa kristu kwa kukumbatia msamaha na maridhiano kwa faida ya mshikamano wa taifa.
Akiongoza wakristu kuadhimisha ijumaa kuu katika jimbo kuu katoliki hilo askofu huyo mstaafu amesema kuwa huu ni wakati wa wakenya tofauti zao za kisiasa na hata za kikabila akisema kuwa ukosefu wa mshikamano wa kitaifa utatumbukiza taifa katika lindi la umaskini.
Askofu Kairo ametoa wito kwa muungano wa madaktari nchini KMPDU na serikali kushiriki mazungumzo kama njia moja ya kuwakwamua wakenya ambao wanaendelea kuhangaika kutafuta huduma za matibabu kufuatia mgomo wa madaktari nchini