Askofu Msaidizi wa jimbo la Eldoret

Baba mtakatifu Francisko amemteua padre John Kiplimo Lelei kuwa askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret.

Tangazo hilo limetolewa na balozi wa Baba mtakatifu hapa nchini na Sudan Kusini Bert Van Megen akisema kuwa hilo lilifuatia ombi la askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich kutokana na ukubwa wa jimbo na kazi ya kitume.

Naye askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amemshukuru Baba Mtakatifu Francisco kwa kuridhia ombi lake akisema kuwa uteuzi huo utarahisisha kazi ya  uinjilishaji katika jimbo.

Askofu mteule John Kiplimo Lelei amehaidi kushirikiana na askofu wa jimbo ili kifanikisha uinjilishaji katika jimbo.

Monsinyo John Kiplimo alizaliwa  1958 katika eneo la Soy, kaunti ya Uasin Gishu jimbo katoliki la Eldoret.

Alijiunga na seminari ya mt.Agostino Mabanga alikosomea falsafa kuanzia mwaka wa 1979-1981 na kati ya mwaka wa 1981-1985 akasomea somo la tiolojia katika seminari kuu ya Mt.Tomaso wa Akwino Langa’ata na baada ya masomo na majiundo akapata daraja la Upadirisho mwaka wa 1985.

Hadi kuteuliwa kwake Monsinyo Kiplimo Lelei amekua akihudumu kama padre mkuu jimbo katoliki la Eldoret baada ya kuteuliwa katika wadhifa huo na askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich mnamo tarehe 28th Agosti 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *