Padre Charles Mutai akumbukwa

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameongoza misa ya kumbukumbu ya siku arobaini ya padre Charles Mutai katika parokia wa mama wa Ludi Turbo.

Kwenye homilia yake katika misa hiyo askofu Dominic Kimengich ametoa wito kwa wakristu kuwa wanyenyekevu akisema kuwa njia moja ya kuurithi ufalme wa mbingu ni unyenyekevu na kuwa na roho wa msamaha.

Askofu ametaka kila mkristu kuwa dhabiti katika imani akisema kuwa njia moja tu ya kuwa na matumaini baada ya kuondoka hapa ulimwengu ni imani dhabiti kwake kristu.

Askofu kadhalika ametoa wito kwa familia nzima ya jimbo katoliki la Eldoret kuzidi kuiombea familia ya padre mwendazake Charles Mutai ili mwenyezi Mungu azidi kuwapa neema.

Ikumbukwe kuwa padre Charles Mutai aliaga dunia mapema mwaka huu usingizini akiwa paroko wa parokia ya mtakatifu Maria Kabisaga na kuzikwa katika maziara ya mapadre iliyoko katika parokia ya mama wa Ludi Turbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *