Murkomen; Miundo msingi kuboreshwa Kerio Valley

Waziri wa barabara na uchukuzi Kipchumba Murkomen sasa anasema kuwa njia mwafaka wa kumaliza utovu wa usalama katika bonde la Kerio ni kuimarisha miundo msingi.

Kwa mujibu wa Murkomen kudorora kwa usalama kumechangiwa na ukosefu wa miundo msingi bora, ili kuwawezesha maafisa wa usalama kutekeleza shuguli zao katika maeneo hayo kikamilifu.

INSERT  MURKOMEN

Murkonen ametoa hakikisho la serikali kuwa swala la utovu wa usalama katika eneo hilo litazikwa katika kaburi la sahau katika siku za hivi karibuni.

Eneo hilo limekumbwa na utovu wa usalama kwa muda mrefu huku serikali ikiratibu mikakati kadhaa ya kusuluhisha tatizo hilo, Murkomen akisema kuwa njia mojawapo ni utengenezaji wa barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *