Eneo pana la bonde la ufa linatarajiwa kunufaika zaidi kufuati a hatua ya shirika la ndege la Kenya airways kurejelea safari zake katika uwanja wa kimataifa ndege wa Eldoret.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa safari hizo gavana wa kaunti ya Elgeiyo Marakwet Wesley Rotich amesema kuwa kurejelewa kwa safari hizo kutapiga jeki sekta ya utalii katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet.
Gavana huyo kadhalika ametoa wito kwa shirika hilo la ndege kuanza huduma za shehena ili kuwanufaisha wafanyibiashara katika eneo la bonde la ufa kupata nafasi ya soko na kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi.
Naye gavana wa kaunti ya Uasin gishu Jonathan Bii Chelilim amesema kuwa kurejea kwa safari hizo za ndege zitawawezesha wawekezaji kutoka katika mataifa mbalimbali kuwekeza katika eneo la bonde la ufa hatua ambayo anasema kuwa itabuni nafasi za ajira.