KCCB; Siki ya mgomo ni chungu kwa wakenya

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini KCCB, limetoa wito wa kuwepo kwa amani kati ya serikali na madaktari wanaogoma kwa siku ya kumi na moja hii leo ili kumaliza mateso ya wagonjwa kote nchini.

Baraza hilo chini ya uenyekiti wa askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde limesema kuwa misimamo mikali inayoshuhudiwa baina ya muungano wa KMPDU na serikali utapelekea wakenya wengi kupoteza maisha yao likitoa wito wa pande hizo mbili kulegeza misimamo.

Kuhusu visa vya ajali barabarani vinavyoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini askofu mkuu Kivuva ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu na kufuata kikamilifu sheria za trafiki ili kuepukana na ajali hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *