Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 25 anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu baada yake kumdunga kisu na kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 24 katika mtaa wa kipkaren viungani mwa mji wa Eldoret kutokana na mzozo wa kinyumbani
Inadaiwa kwamba felix Anunda walikosana na mkewe Dorcas Ntinyari kwenye nyumba yao katika eneo la kisumu.ndogo katika mtaa wa Langas na akaweza kutorokea kwa dadake katika mtaa jirani wa kipkaren
Anunda anadaiwa kumfuata marehemu kwa nyumba hiyo akitaka kuchukua mavazi na kibeti alivyokua amemnunulia ambapo alimpata akikatakata mboga na baada yao kuvutana, mshukiwa anadaiwa kuchukua kisu kilichotumika kukata mboga na kumdunga Ntinyari mara moja tumboni na akafariki papo hapo.
Akithibitisha haya kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kapseret Sarah Chepkoech amesema kwamba polisi waliweza kumkamata mshukiwa na kwamba atafukishwa kortini kufunguliwa mashtaka pindi uchunguzi utakapokamilika.
Chepkoech ameongeza kwamba maiti ya mwendazake ilihamishiwa katika hifadhi ya hospitali ya mafunzo na rufaa ya moi Eldoret ( mtrh).