kilimo cha chakula cha mifugo

Wito umetolewa kwa wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu wamehimizwa kukumbatia kilimo biashara ili kuimarisha mapato yao.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake waziri wa kilimo, ustawi wa mifugo na uvuvi kaunti ya uasin gishu Edward Sawe, amewarai wakazi kupanda mimea inayochukua muda mfupi kukomaa ili kuongeza kapu la chakula kadhalika kupata mapato zaidi.

Wakati uo huo Sawe amefichua kuwa serikali ya kuanti imeanzisha mpango wa kuwapa wakulima mbegu za alizeti [sunflower) bila malipo huku pia akiwataka wakulima kujisajili ili kunufaika na mbolea ya bei nafuu kutoka kwa serikali ya kitaifa.

Aidha, waziri huyo wa kaunti amewahimiza endelea kuwashauri wakulima wa mahindi na ngano kuvuna mazao yao mapema ili kuepuka hasara wakati huu wa mvua nyingi.

Amedokeza kuwa kaunti inatarajia kupata mashine 12 za kukausha nafaka kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *