Muungano wa wanaopanga miji nchini ( town planners association ) wamelalamikia unyakuzi wa ardhi ya umma wakiutaja kama changamoto kuu kwa ukuaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye miji mingi nchini.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano huo nchini mairura Omwenga, muungano huo unapendekeza sheria kutekelezwa ili kuwezesha ubomoaji wa katika ardhi ya umma ili miradi iweze kutekelezwa katika maeneo ambapo imetengewa kufanyika bila ugumu wowote .
Wakizungumza kwenye mkutano wao wa kila mwaka mjini Eldoret wanasema maendeleo yataweza kutekelezwa katika maeneo ya miji iwapo masuala mbalimbali yakiwemo unyakuzi wa ardhi yataweza kutiliwa maanani.