Kundi la mashabiki wa idhaa hii ya Upendo
linalofahamika kama St John’s Bwamwai Salaams club, limesherekea mwaka mmoja
hii leo tangu kubuniwa kwake katika eneo la St Anne’s Kapkures kaunti ya Elgeyo
Marakwet.
Akiongoza hafla ya Misa ya sherehe hiyo, padre Fredrick Ng’elechei amewahimiza wakristu kuimarisha na kujenga msingi dhabiti na imara ya imani kwa kuwa hio ndio nguzo kuu ya mafanikio na maendeleo katika maisha ya mkristu.
Padre Ng’elechei amewakumbusha wakristo kuwa safari ya imani ni juhudi na bidii ya mhusika katika hatua za maisha ikiwa ni katika koo za jamii.
Wakti huo padre Ng’elechei ametoa wito kwa wakristo katika kipindi hichi cha maajilio kubadili mienendo na kumwongokea mwenyezi mungu kupitia toba