Wanapatholojia wabaini kilichomuua Tob Cohen

Wanapatholojia walioupasua mwili wa mfanyabiashara raia wa Uholanzi Tob Cohen, wamedokeza kwamba tayari wamebaini kilichomuua Cohen japo ila hawataweka wazi kwa umma matokeo hayo kutokana na agizo la mahakama.

Shughuli hiyo iliendeshwa jana kwa zaidi ya saa nne na kuongozwa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali, Dkt. Johansen Oduor ambaye alisema kwamba tayari wamebaini alivyouliwa.

Upasuaji huyo ulifanyika wakati mzozo wa nani anayepaswa kumzika marehemu ukitarajiwa kutatuliwa baadaye leo baada ya mshukiwa mkuu wa mauaji yake ambaye pia ni mkewe Sarah Wairimu kuitaka Hifadhi ya Maiti ya Chiromo kuzuia mwili huo kuchukuliwa na nduguze Cohen. Sarah Cohen alisisitiza jana kwamba yeye ndiye mwenye haki ya kuuchukua mwili huo.

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "Wanapatholojia wabaini kilichomuua Tob Cohen"

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email