Peter Chomba; Usalama Uimarishwe Eldoret.

Mwakilishi wa wadi ya Huruma kaunti ya Uasin Gishu Peter Chomba, ametoa wito kwa idara ya usalama kaunti hii kumakinika na kukabili visa vya uhalifu anavyosema vimekithiri eneo hilo.

Chomba amesema wakazi wa eneo hilo wameanza kuingiwa na hofu ya kuvamiwa na hata nyumba zao kuvunjwa majira ya usiku huku akihusisha visa hivyo na kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya.

Mwakilishi huyo wa Wadi sasa anamwomba kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu kufanikisha juhudi za kujenga kituo cha polisi kwenye ardhi anayosema ilitolewa kwa hilo ili kukabili utovu wa usalama katika wadi hiyo.

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "Peter Chomba; Usalama Uimarishwe Eldoret."

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email