Bishop Crowley; komesheni uaviaji mimba

Red stop sign. Stop abortion text.

Red stop sign. Stop abortion text.

Askofu msimamizi wa jimbo hili la Eldoret askofu Maurice Anthony Crowley amewaonya wansiasa dhidi ya kupitisha miswada itakayoidhinisha uavyaji wa mimba akisema kuwa uuaji ni kinyume na amri za mungu.

Askofu Crowley amesema hayo hii leo katika parokia ya Narkwo kwenye misa maalum iliyoandaliwa kwa ajili wa watoto walio na changamoto za kimaumbile katika parokia hiyo almaarufu Nerkwo small home akihimiza wazazi na wakristu kwa ujumla kujitokeza kuwasaidia watoto hao kwa hali na mali pasi na kuwabagua.

Kadhalika amewataka wazazi kuchukua nafasi yao katika familia na jamii ili kuhakikisha kuwa jamii na hasa watoto wanakuwa na maadili mema na kuwatakia watahiniwa wote wanaotarajia kufanya mtihani wa kitaifa heri njema.

 

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "Bishop Crowley; komesheni uaviaji mimba"

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email