BISHOP CROWLEY: Acheni Malumbano Ya Kisiasa

Wito umetolewa kwa wanasiasa wa bonde la ufa kukomesha siasa na badala yake kushughulika na maswala yatakayowafaidi wananchi.

Wito huo umetolewa na askofu msimamizi wa jimbo hili la Eldoret askofu Maurice Anthony Crowley  hii leo kwenye misa ya ufunguzi wa kanisa jipya la mama wa Fatima Moiben akisema kuwa umoja na ushirikiano baina ya viongozi ndio utakaofanikisha utendakazi kwa wananchi.

Baadhi viongozi ambao wamehudhuria hafla ya ufunguzi wa kanisa hilo ni Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Chemelil Zedekiah Bundotich mbunge wa Moiben Sila Tiren miongoni mwa viongozi wengine

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "BISHOP CROWLEY: Acheni Malumbano Ya Kisiasa"

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email