Margaret Kenyatta; Tuboreshe Maisha Ya Vijana na Watoto.

Mama wa Taifa Margaret Kenyatta amewataka Wakenya ikiwemo mashirika ya serikali na yale yasio ya kiserikali kutekeleza mipango inayokusudiwa kuboresha maisha ya vijana na watoto.

Alisema mipango ya maendeleo ya kijamii ambayo inasaidia kukuza na kuimarisha vipawa vya watoto yapaswa kustawishwa zaidi kuwafikia watoto na vijana wengi zaidi kote nchini.

Mama wa Taifa aliyasema haya alipotembelea mpango wa kukuza vipawa vya muziki miongoni mwa watoto na vijana unaotambulika kama Ghetto Classics ulioko kanisa katoliki la St. John’s, mtaa wa Korogocho, katika kaunti ya Nairobi.

Ghetto Classics ni mpango wa Wakfu wa Usanii wa Muziki ambao kwanza ulianzishwa katika mtaa wa Korogocho mwaka wa 2009 lakini sasa umesambazwa katika kaunti mbali mbali huku ukinufaisha zaidi ya watoto na vijana wapatao 1,500.

Amewahimiza waanzilishi wa mradi huu kusajili watoto na vijana zaidi akisema utawasaidia kuwaepusha vijana wanaobalehe na maovu ya kijamii na kuwaelekeza katika njia sawa ya maisha.

Alipongeza Parokia ya Kanisa Katoliki ya Kariobangi na jamii ya Korogocho kwa kuandaa mpango huo akidokeza kwamba umekuwa sehemu muhimu ya jamii.

Balozi Mohammed alipongeza watoto na vijana wa Korogocho kwa kuchagua kubadilisha maisha yao kwa kuwa sehemu ya Mpango wa Ghetto Classics.

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "Margaret Kenyatta; Tuboreshe Maisha Ya Vijana na Watoto."

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email