Gavana Kimemia Awafuta Kazi Mawaziri

Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia amewafuta kazi Mawaziri wanne saa chache tu baada ya kikao cha kuangazia utendakazi wa mawaziri kwa muda wa miaka miwili ambayo amehudumu kukamilika.

Wanne hao wametimuliwa usiku wa manane leo hii, dakika chache tu baada ya kuondoka katika kikao baina yao na Gavana Kimemia katika makao makuu mjini Ol Kalou.

Shoka hilo la Kimemia limewaangukia Mawaziri wa Maji, Simon Ng’ang’a, Muthoni Wamuiya wa biashara na ushirika, Faith Mbugua wa elimu na Kariuki Mbataru wa Utawala wa Umma.

Mbataru tayari alikuwa anakabiliwa na tishio la kubanduliwa afisini baada ya hoja ya kutokuwa na imani naye kuhajadiliwa bungeni akihusishwa na utovu wa maadili.

Gavana Kimemia aidha amesema kwamba kutimuliwa kwao afisini kunalenga kuimarisha utaoji huduma kwa wananchi huku akisema kamwe hatawavumilia maafisa wazembe katika serikali yake.

Please follow and like us:
error

Be the first to comment on "Gavana Kimemia Awafuta Kazi Mawaziri"

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


Facebook189
Twitter38
Google+
Follow by Email